Wednesday, May 14, 2008

Miss Tanga 2008 lapata Wadhamini Wapya

Kampuni ya Tanga Fresh yaipiga tafu Miss Tanga 2008

MCHUANO wa kumsaka Kisura wa Tanga ndio kama hivyo umekwishaanza kutimua vumbi lake, huku kampuni mbalimbali zikithibitisha udhamini wao. Kampuni ya Maziwa ya Tanga Fresh Limited nayo imetangaza udhamini mnono.

Meneja Mwandamizi wa kampuni hiyo Alnoor Hussein inayozalisha aina mbalimbali za maziwa, maziwa ya mgando na jibini alisema kampuni yao imejikita kudhamini mashindano hayo ikiwa ni mkakati wa kampuni yake kuzitangaza bidhaa zake kupitia mashindano kama haya katika kuhimiza matumizi ya maziwa kama njia ya kuboresha afya na nguvu katika miili na pia kuipa sapoti michuano hiyo.

Alnoor aliwataka wadhamini wengine wajitokeze ili kudhamini mashindano hayo ili kuboresha zaidi akisema kuwa mashindano kama haya yanatoa ajira kwa wasichana ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha yao na kuwajengea kujiamini.
Alisema pamoja na udhamini huo, warembo watapapewa bidhaa zake kwa ajili ya kuimarisha ngozi zao pamoja na kupata fursa ya kufanya ziara katika kiwanda hicho bora cha maziwa nchini ili kuona jinsi wanavyoendesha shughuli zao.


Hoteli mpya na ya Kisasa Tanga. Inasemekana ni Hotel pekee mjini Tanga ambayo itakuwa inatumia kadi kufungua milango. Regal Naivera Hotel wamejitokeza kudhamini miss Tanga 2008.









KARATA CLASSIC FURNITURE
"Where Confrotability & Durability meet?"

Kampuni ya Karata classic furniture iliyoko maeneo ya Taifa Road, Mkabala na Mabanda ya Papa kwenye kona ya kuingia soko la Mgandini jijini Tanga ni moja ya wadhamni wa Miss Tanga 2008.


Kampuni hii bingwa wa furniture wanatengeneza kila aina ya sofa, vitanda, na meza za chakula, yaani furniture zote za living Room, Dinning Room, Bed Room na Ofisini kwa dizaini ya kisasa na zilizotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu na za uhakika zaidi.


Karata Classic Furniture ni suluhisho la thamani za majumbani na ofisini pia.


Kwa mahitaji yako wasiliana nao kwa: 0754 148 169 na 0717 906 567 au kwa barua pepe: karatafurniture@gmail.com