Wednesday, April 30, 2008

Mchaka mchaka Miss Tanga Umeanza

MISS VYUO NAO HAO....
Jumla ya Warembo 10 wamejitokeza kuwania nafasi za kujikita Miss Tanga kupitia taji la Miss Collage. Watano kati ya hao wataingia moja kwa moja kambi ya miss Tanga wakiwa na wenzao kutoka miss Usagara, Miss Korogwe na Miss Lushoto. Taji la Miss Collage mpaka sasa limeshikiliwa na Victoria Martin ambaye pia ni Miss Tanga, Miss Kanda ya Kaskazini na Balozi wa Redds 2007.
Mwaka jana ilikuwa hivi: Mratibu wa shindano la Miss College 2008, Maximilian Luhanga ambaye pia ni Mkurugenzi wa New Face Entertenment iliyopewa dhamana ya kuandaa kitogoji hicho alisema onyesho litafanyika Habours Club jijini Tanga. Miss collage 2008 limedhaminiwa na Redds, Mwananchi Communication, Golden Pulm Café, Sofia Records na Mwambao FM.

Wanaochuana kuwania taji hilo ni Mariam Hajibu, Beatrice Liwemba, Evelyne Balozi, Mwajuma Msangi, Mariam Mhando, Silvia Urio, Dorice Steven, Mwanamina Bausi, Halima Khalfan na Agnes Mwakipesile, kama wanavyoonekana pichani chini.

Mshindi wa kwanza atajinyakulia seti ya Televisen, wa pili na wa tatu watapewa simu za mkononi wakati watakaoshika nafasi ya nne hadi 10 watapata fursa ya kufunguliwa akaunti katika benki ya Backleys Jijini hapa.

Na mshindi ni...!



MISS USAGARA JUKWAANI...
MBIO za kumsaka mrembo wa Tanga zimeanza! Jumla ya warembo 9 walipanda jukwaani kuchuana kuwania nafasi za kushiriki katika shindano la Miss Tanga kupitia kitogoji cha Miss Usagara, ambapo tano bora ya warembo hao watapata tiketi ya moja kwa moja kuingia katika fainali za Miss Tanga 2008.

Kitongoji hicho cha kwanza kufanyika Miss Usagara 2008, kimefanyika Mei 2 katika Ukumbi wa Splended Jijini hapa, ambapo mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini anayetamba kwa sasa na wimbo wake Ni Soo!, Haji Mtepa al'maarufu kwa jina la Pasha ndiye aliyetifua vumbi usiku huo katika kinyang'anyiro hicho.

Onyesho hilo linaratibiwa na Lilian Kihama Maim kupitia kampuni yake ya Sunrise Secretarial & Beauty Saloon na limefanyika katika Ukumbi wa Splended Jijini hapa.
Warembo hao tisa walikuwa ni pamoja na Aisha Abdallah, Judith Asei, Hawa Njama, Amina Sadik, Khadija Ramadhani, Salma Mohamed, Merry Fedrick, Oliva Mango na Nuru Sheshe.

Judith Assey ndiye aliyetwaa taji la Miss Usagara 2008.

Mshindi wa pili kulia ni Oliver Mango na mshindi wa tatu kushoto ni Nuru Salim. Aliyevikwa taji la Mwenye kipaji kwa warembo wa Usagara ni Amina Sadick na taji la tabia njema lilikwenda kwa Hadija Ramadhani Kulia. Tano bora ya miss usagara inaingia moja kwa moja katika fainali za Miss Tanga 2008.

MIss Lushoto nayo hiyo..

Wednesday, April 23, 2008

Beauty with Purpose



Baada ya kuvikwa mataji ya Miss Tanga, Dollywood Miss Photogenic, Miss Kanda ya Kaskazini, Miss Redds Fashion Ambassador Victoria Martin hivi karibuni alichaguliwa pia kukampeni dhidi ya ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wanawake na chama cha wanawake waathirika wa ugonjwa wa saratani ya matiti Tanzania. chama hicho kina lenga kusaidia wanawake wenzao kwa kuwapa mawaidha na kuwasaidia kwa matibabu ambayo yanasemekana kuwa ya ghali na kuwapatia matiti bandia n.k. Kama unataka kusaidia piga simu namba 0713 711413 tutakuunganisha. Pichani ni Victoria akitoa misaada kwa wanawake walioathirika na ugonjwa wa kansa (Saratani) katika siku ya wapendanao duniani, kama namna ya kuonyesha ishara ya upendo.

Breaking The Good News...


Miss Tanga2007, Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini, Redds fashion Ambassador Victoria Martin akiongea na mwandishi wa habari kuhusu mikataba yake na kampuni za Modelling za South Afika. Vicky hivi karibuni alikwenda South Afica kuangalia soko la uanamitindo na tayari kampuni mbili zimevutiwa naye na kumpa mapendekezo yao. Kampuni hizo ni O Model na EXTRA.

Mshindi wa shindano la Big Bro Africa II 2007 Tatiana Durao akiwa amepozi na balozi wa Redds Victoria Martin leo asubuhi ndani ya hoteli ya Movenpick baada ya kuwasili kwa ajili ya kuongea na waandishi wa habari kuhusu maonyesho ya mavazi nchini.


Hapa wanafurahia jambo



Vicky ampokea Tatiana


Mshindi wa tatu wa shindano la Big Brother Africa II mwaka 2007 Tatiana Durao akiwa airport baada ya kupokelewa na balozi wa Redds, Miss Tanga 2007, Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini Victoria Martin baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere jana kwa ajili ya maonyesho mawili ya mavazi. Guess who? amepagwa kuchill naye akiwa bongo.... Vicky.

KAZI ZA KIJAMII

PONGEZI:
Victoria Martin akiwapongoza wakina mama waliojifungua siku ya mkesha wa siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 8 March





Nasi mkuu wa Hospitali ya Agakhan akishukuru mbele ya vyombo vya habari kwa kutembelewa hospitalini hapo na kwa zawadi.


MSAADA:

Victoria na wengine na Watoto yatima wa Tanzania Mitindo House


Miss Tanga, Balozi wa Redds Victoria Martin akimkabidhi mgeni rasmi Mama Anna Kilango kiasi cha shilingi laki mbili cash ikiwa ni moja ya mchango wake katika kukizindia kituo cha watoto yatima cha (Tanzania Mitindo House) kilichoasisiwa na Khadija Mwanamboka na wenzake.

Thursday, April 17, 2008

Tuzo za Redds kwa wanawake wataftaji (Febr. 8)

Walio zawadiwa ni pamoja na:

Rita Palson


Khadija Mwanamboka


Fina Mango


Nancy sumari


Jokate Mwegelo


Lady Jay Dee


Sofia Bianaku

Hii ilikuwa ni katika kuadhimisha siku ya wapendanao duniani mwaka huu ambapo Balozi wa Redds Victoria Martin kupita Redds aliwakabidhi zawadi za kuwatunuku tuzo ya utambuzi wa kazi na mafanikio ya kila mwanamke mtajwa hapo juu na wengine. Kushuhudia zoezi hili ni Mr Mpeli Nsekela.

FAIDIKA

Miss Tanga 2008 ....?


Tukiwa tunasubiri kwa hamu kuanza kwa mchakato wa miss tanga 2008 faidika na promoshen za vodacom ambao ndio wadhamini wa kuu wa mashindano haya. kazi kwako



Tuesday, April 8, 2008

Miss Tanga 2008



TAARIFA YA MKURUGENZI

MASHINDANO ya urembo kumsaka kisura wa Tanga (Miss Tanga 2008) yatakujia kupitia kampuni ya Five Brothers Entertainment yenye makazi yake jijini Tanga. Kampuni hii inachukua jukumu hili zito ikiwa ni mara nyingine tena katika historia ya mashindano haya hapa nchini.

Mwaka Jana kama utavuta kumbukumbu zako vizuri utakumbuka kuwa, tulifanikiwa kwa kiasi kikubwa kufikia malengo yetu kwa kumpata mrembo aliyetikisa katika kilele cha mashindano ya Miss Tanzania na hatimaye kufanikiwa kunyakua taji la Ubalozi wa Mitindo wa Redds, naye si mwingine zaidi ya VICTORIA MARTIN.

Hapa napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa Victoria Mwenyewe kwa juhudi zake alizozionyesha katika kipindi chake, Vyombo vya Habari, Kamati ya Miss Tanzania, Kampuni ya Redds na Wadau walioshiriki kwa namna moja ama nyingine, bila kuwasahau mashabiki na yeyote ambaye ingestahiki kupata pongezi hizi, japo kimya kimya.

Lengo letu hasa ni kuonyesha utofauti uliopo kutoka kwetu na wengine na safari hii tunataka kuhakikisha kuwa Tanga inatoa wawakilishi walioandaliwa vema, wanaoweza kutoa changamoto katika mashindano ya dunia. Ni kweli tumedhamiria kushinda taji la taifa na mrembo wetu kufanya maajabu ambayo hayajawahi kufanywa katika mashindano ya urembo, Miss World 2008.

Malengo haya ni mazito na hayawezi kukamilika bila ushirikiano wako wewe. Kwanza kabisa binti yeyote mwenye kipaji na nia ya kuishi maisha yake katika fani ya urembo. Pili, familia ya binti huyo kwa kutoa sapoti kwa binti yako kushiriki katika kufanikisha azma ya kipaji chake. Tatu, kwako wewe mdau wa mashindano haya ya urembo kushirikiana nasi katika zoezi hili la kuwapata wawakilishi bora kwa namna unayoweza na sapoti unayoweza kutoa ili kutimiza adhma hii.

Labda nikupashe tu kidogo kuwa, Kampuni ya Five Brothers Entertainment inahusika na utayarishaji wa matamasha mbalimbali. Tunao uzoefu wa kutosha katika shughuli hizi hapa nchini na hii ni fursa adimu na muhimu kwako kushiririkiana nasi kama unataka kujitangaza ama kufanya kazi nasi.

Inaweza pia kuwa fursa ya kubadilishana uzoefu, kufahamiana na pia kupata kazi za matunda ya kampuni yetu. Huu ni wito na mwanzo mwema wa kujenga ushirikiano wetu kwako na kwako kwetu. Tunaamini kuwa ushirikiano huu utazidi kuanzia hapa ambapo utapata fursa ya kutumia huduma zetu na sisi kuendelea kukuthamini kama mtumiaji huduma mwenye taadhima zote.

Shangamoto zaidi ni kwa Masponsor (Wadhamini wa shughuli hizi), wakati bendera ya mrembo wetu ikipepea, nao watapepea pia, Hapa tunapenda kuwashukuru wadhamini ambao tayari wamekwisha jitokeza ikiwa ni pamoja na Vodacom Tanzania, ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano haya, Redds Premium cold, CRDB Bank-Tanga Branch, Hotel Kola Prieto, Sofia Productions, Vayle spring, JD's Entertainment, DOLLYWOOD TZ na Gazeti la Jahazi. Tunasubiri kwa hamu kuwatangaza zaidi na kuendelea kuelimisha jamii kuhusu huduma zenu bora. Tunaacha njia zetu za mawasiliano wazi kwa yeyote anayetaka kudhamini na kufaidika na mpango huu, ...unaweza kuwasiliana nasi kupitia 0713 711413

Kupitia Gazeti Tando hili, tutatoa pia fursa kwako msomaji kutoa ushauri, mtazamo na maoni ya mambo mbalimbali. Inaweza kuwa, kutuomba tuwashauri mabinti unaowafahamu ili washiriki katika shindano hili, inaweza kuwa maoni kwa ajili ya mchakato wetu na pia kupitia blog hii tutakupa kila hatua ya shindano hili la kumsaka Miss Tanga 2008 litakavyokwenda. Kama utakuwa na maswali kwa washiriki au sisi waandaaji utatakiwa kutoa maswali yako pia hapa ukifuatia njia nyingine kama e-mail (asmahmakau@yahoo.co.in) na barua (Kwa Mkurugenzi, 5brothers Entertaiment, 14036DSM.

Ninakukaribisha sana, shiriki nasi katika kuipa Tanga ramani yake na heshima inayostahili, hapa Tanzania na duniani kote. Ahsante sana na karibu! :-)