Tuesday, April 8, 2008

Miss Tanga 2008



TAARIFA YA MKURUGENZI

MASHINDANO ya urembo kumsaka kisura wa Tanga (Miss Tanga 2008) yatakujia kupitia kampuni ya Five Brothers Entertainment yenye makazi yake jijini Tanga. Kampuni hii inachukua jukumu hili zito ikiwa ni mara nyingine tena katika historia ya mashindano haya hapa nchini.

Mwaka Jana kama utavuta kumbukumbu zako vizuri utakumbuka kuwa, tulifanikiwa kwa kiasi kikubwa kufikia malengo yetu kwa kumpata mrembo aliyetikisa katika kilele cha mashindano ya Miss Tanzania na hatimaye kufanikiwa kunyakua taji la Ubalozi wa Mitindo wa Redds, naye si mwingine zaidi ya VICTORIA MARTIN.

Hapa napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa Victoria Mwenyewe kwa juhudi zake alizozionyesha katika kipindi chake, Vyombo vya Habari, Kamati ya Miss Tanzania, Kampuni ya Redds na Wadau walioshiriki kwa namna moja ama nyingine, bila kuwasahau mashabiki na yeyote ambaye ingestahiki kupata pongezi hizi, japo kimya kimya.

Lengo letu hasa ni kuonyesha utofauti uliopo kutoka kwetu na wengine na safari hii tunataka kuhakikisha kuwa Tanga inatoa wawakilishi walioandaliwa vema, wanaoweza kutoa changamoto katika mashindano ya dunia. Ni kweli tumedhamiria kushinda taji la taifa na mrembo wetu kufanya maajabu ambayo hayajawahi kufanywa katika mashindano ya urembo, Miss World 2008.

Malengo haya ni mazito na hayawezi kukamilika bila ushirikiano wako wewe. Kwanza kabisa binti yeyote mwenye kipaji na nia ya kuishi maisha yake katika fani ya urembo. Pili, familia ya binti huyo kwa kutoa sapoti kwa binti yako kushiriki katika kufanikisha azma ya kipaji chake. Tatu, kwako wewe mdau wa mashindano haya ya urembo kushirikiana nasi katika zoezi hili la kuwapata wawakilishi bora kwa namna unayoweza na sapoti unayoweza kutoa ili kutimiza adhma hii.

Labda nikupashe tu kidogo kuwa, Kampuni ya Five Brothers Entertainment inahusika na utayarishaji wa matamasha mbalimbali. Tunao uzoefu wa kutosha katika shughuli hizi hapa nchini na hii ni fursa adimu na muhimu kwako kushiririkiana nasi kama unataka kujitangaza ama kufanya kazi nasi.

Inaweza pia kuwa fursa ya kubadilishana uzoefu, kufahamiana na pia kupata kazi za matunda ya kampuni yetu. Huu ni wito na mwanzo mwema wa kujenga ushirikiano wetu kwako na kwako kwetu. Tunaamini kuwa ushirikiano huu utazidi kuanzia hapa ambapo utapata fursa ya kutumia huduma zetu na sisi kuendelea kukuthamini kama mtumiaji huduma mwenye taadhima zote.

Shangamoto zaidi ni kwa Masponsor (Wadhamini wa shughuli hizi), wakati bendera ya mrembo wetu ikipepea, nao watapepea pia, Hapa tunapenda kuwashukuru wadhamini ambao tayari wamekwisha jitokeza ikiwa ni pamoja na Vodacom Tanzania, ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano haya, Redds Premium cold, CRDB Bank-Tanga Branch, Hotel Kola Prieto, Sofia Productions, Vayle spring, JD's Entertainment, DOLLYWOOD TZ na Gazeti la Jahazi. Tunasubiri kwa hamu kuwatangaza zaidi na kuendelea kuelimisha jamii kuhusu huduma zenu bora. Tunaacha njia zetu za mawasiliano wazi kwa yeyote anayetaka kudhamini na kufaidika na mpango huu, ...unaweza kuwasiliana nasi kupitia 0713 711413

Kupitia Gazeti Tando hili, tutatoa pia fursa kwako msomaji kutoa ushauri, mtazamo na maoni ya mambo mbalimbali. Inaweza kuwa, kutuomba tuwashauri mabinti unaowafahamu ili washiriki katika shindano hili, inaweza kuwa maoni kwa ajili ya mchakato wetu na pia kupitia blog hii tutakupa kila hatua ya shindano hili la kumsaka Miss Tanga 2008 litakavyokwenda. Kama utakuwa na maswali kwa washiriki au sisi waandaaji utatakiwa kutoa maswali yako pia hapa ukifuatia njia nyingine kama e-mail (asmahmakau@yahoo.co.in) na barua (Kwa Mkurugenzi, 5brothers Entertaiment, 14036DSM.

Ninakukaribisha sana, shiriki nasi katika kuipa Tanga ramani yake na heshima inayostahili, hapa Tanzania na duniani kote. Ahsante sana na karibu! :-)

No comments: